Jump to content

User:Dilemma teknix- D tek

From Wikipedia, the free encyclopedia

Jina halisi ni Faraji Issa Said mzaliwa wa Kigoma pale Bangwe na alianza harakati za sanaa akiwa kidato cha pili pale Shy bush maeneo ya Mwadui kwa utunzi wa mashairi japokuwa hakuwa akighani. Alifahamika kwa umahiri wa kucheza mpira wa kikapu pale Risasi na B4 mwadui.Sanaa rasmi alianza pale Kimara mwaka 2009 akiwa na Nod Mkombozi sasa yuko Mawehu productions akiwa na marehemu PopJ pia shule moja. 2010 alijiunga na Chuo cha Mipango Dodoma pale akakutana na Boniphace Magayane a.k.a Bonito ambaye awali walikutana kwenye masomo ya ziada Dar-Ubungo na waligundua kuwa kila mmoja alikua na kitu katika sanaa.Wakati huohuo Dilemma alikutana na Adam Shule Kongwe na kuanza kupeana ujuzi zaidi kuhusu kughani kabla ya watatu hao kuanza kukaa pamoja na kubadilishana mawazo kuhusu sanaa. Gheto kwa Dilemma ndiyo palikuwa maskani na washkaji wengine wengi tu walikuja na kusikiliza wakichana kwenye midundo ya mbele. Dilemma aliamua kuanza kurecord kwa kutumia laptop yake na walirecord mixtape ya kwanza iliyoitwa Plannaz Anthem ikiwa na nyimbo kama Na na na na nyimbo nyingine kibao kabla ya kurecord mixtape ya pili iliyoitwa Pure hedonistic wakiwa na Lewisky, Goda Mc, Maseke, Jesus. 2012 Dilemma aliamua kufanya kazi za pekee na kuandaa mixtape yake iliyoitwa M.Y.M.F yaani Majumuisho ya mpango flani ambayo ilikuwa na nyimbo kama Dope, Shabiki, Game inaenda vipi, Girlfriend, bora nisiwe star,unarusha stimu na nyingine kibao tu zikifanywa na watayarishaji kadhaa kama Willa touchez,Nottty,Mab j na Stim master. 2013 kuelekea kumaliza Chuo alipumzika kufanya muziki na kuanza kusaport zaidi vijana wanaofanya ikiwemo kujiandaa katika utayarishaji muziki pia. Washkaji walianza kukutana Maili mbili ghetto kwa Goda Mc huko alikuwepo LC - lucas Malali ambapo waliendeleza harakati za kurecord kama solo kila mtu kabla ya kuamua kurecord pamoja kama kundi na baadae waliliita kundi hilo DDC.